Kuomba ufafanuzi wa Wizara ya Afya ya Tanzania juu Afua za watoto wanaozaliwa jinsi tata

The Issue

Naitwa Baby John Musamba,Mtanzania  mwanaharakati wa haki za binadamu na Mtanzania wa kwanza kusimama  hadhalani kuelezea changamoto wanazopitia watoto wenye jinsi tata Tanzania ambazo hata mimi nimezipitia na hii kunifanya kushindwa kufurahia utoto wangu.

Sikuweza kupata ufafanuzi wa kitaalamu nini hasa nilikuwa napitia kipindi ningali mdogo mpaka nilipofikisha umri wa miaka ishirini(20).

Na hii ilichangiwa na uelewa hafifu kutoka kwa jamii lakini vilevile pamoja na wataalamu wa afya wa kipindi hicho na kuna wengine mpaka sasa hawafahamu kwa undani juu ya hali  hii.

Jinsi tata nini? (Intersex) au Disorder/difference in Sex development

Kwa mujibu wa Shirika linalotetea Watoto na Watu wanaozaliwa na changamoto ya via vya uzazi au jinsi tata, huyu ni mtoto anazaliwa nayo akiwa na mapungufu yanayomfanya kushindwa kupata utambulisho kamili wa jinsi ya kike au kiume na inatokana na changamoto wakati uumbaji au utengeneza viungo vya uzazi vya nje au vya ndani au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa Wataalamu wa vyuo vikuu vya Afya na Tiba hapa nchini,

Jinsi Tata inajumuisha aina mbalimbali za hali ambazo watu wanazaliwa nazo, au kuzipata baadaye maishani, ikiwa ni pamoja na ujazo wa viungo vya uzazi vya nje na/au mchanganyiko wa kromosomu, tezi za uzazi, viungo vya uzazi vya nje, na homoni ambazo hazilingani kama ilivyo kwa kawaida kwa wanaume au wanawake. Audha kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, "hazilingani na dhana mbili za kawaida za mwili wa mwanaume au mwanawake
 
Nimeweza kufanya mambo mbalimbali kwa kushirikiana na wataalamu   kutoa uelewa na elimu kwa watu wa tabaka zote ikiwepo wataalamu na wananchi wa kawaida na hii niliweza kufanya hili kupitia taasisi ya Tanzania Voice of humanity (www.tvoh.or.tz niliianzisha kwa kushirikia na wataalamu wa kada tofauti ili niweze kufikia wigo mpana  zaidi kwa walengwa na jamii kwa ujumla.

Nimeshukuru kupata  ushirikiano wa kutosha kupitia hayo makongamano na washa tofauti tofauti katika kutoa elimu kwenye eneo hili.

Kutokana maelezo hapo juu changamoto  kubwa ni kutokupata   kauli maalumu ya serikali kupitia Wizara ya Afya kuelezea ni Afua(intervention) gani zinaweza kufanyika juu ya watoto wanaozaliwa na hali hii. Ili kuweza kupunguza unyanyapaa mkubwa unaendelea kwenye jamii  pamoja huduma za masahihisho za upasuaji wanazofanyiwa watoto(unnecessary surgery) juu ya hali hii.kama ilivyotolewa ufafanuzi na tume ya haki za binadamu afrika kupitia waraka wa mwaka 2023 kupitia .....

 https://achpr.au.int/en/adopted-resolutions/resolution-promotion-and-protection-rights-intersex-persons

Ukiwa ni sehemu ya jamii hii ningependa unaisidie tuweza kufikisha sahihi(signatures) elfu moja (1000) ili ujumbe wetu uweze kuwafikia wahusika na waweze kutusaidia kwenye hii asante sana kwa kushiriki

avatar of the starter
Baby MusambaPetition StarterI’m Executive Director of Tanzania Voice of Humanity ,wish To improve the welfare of Intersex to make sure they are recognized, economically empowered, well protected and treated through empowerment support.

28

Petition Updates