Tanzania revolution. No TO DICTATORSHIP, YES TO DEMOCRACY

0 have signed. Let’s get to 5,000!


MAANDAMANO NDIO JIBU LA UKOMBOZI WA TAIFA HILI.
Udikteta ni nini? { 1 }Udikteta ni aina ya serikali ambayo nchi au kikundi cha nchi inatawaliwa na chama moja au mtu binafsi (dictator) au kwa uhuru na nguvu hutumiwa kwa njia mbalimbali ili kuhakikisha kwamba nguvu za taasisi zinabakia nguvu.{ 2 } Udikteta ni aina ya uhuru ambapo wanasiasa hutawala karibu kila nyanja ya tabia ya umma na binafsi ya wananchi.{ 3 } Udikteta na jamii za kikatili kwa ujumla hutumia propaganda za kisiasa ili kupunguza ushawishi wa washiriki wa mifumo ya udhibiti mbadala.
Kutokana na hali ya kisiasa nchini{Tanzania}, inayotokana na ukandamizwaji mkubwa wa haki za raia na haki za binadamu.
Kuna haja ya kufanyika kwa maamuzi magumu ya kulikomboa Taifa.
Ukiukwaji huu mkubwa wa haki za watanzania, unao tekelezwa kikamilifu na vyombo vya dola, kwa makusudi na jeuri tu, ni lazima upingwe kwa nguvu zote na wa kuupinga ni sisi watanzania wema.
Mauwaji ya raia wasio na hatia, vifungo vya kisiasa kwasababu tu, wapinzani wamemkosoa au kumpinga Rais, ukosefu wa ajira, kuporomoka kwa uchumi, ubaguzi na chuki zinazo enezwa na watawala na namna ambavyo tumevunjiwa nyumba zetu bila fidia, ni lazima tuamke kama Taifa bila kujali vitisho vyovyote vile kutoka kwenye vyombo vya dola.
Binafsi naunga mkono jitihada zozote zile za maandamano ya amani Tanzania. Yawe ni maandamano ya kumpinga Rais, ninayaunga mkono, yawe ni maandamano ya kumtaka Rais aondoke madarakani, nayo ninayaunga mkono, yawe ni maandamano ya kukiondoa ccm madarakani nayo pia ninayaunga mkono.
Hakuna namna nyingine ya kulikomboa Taifa zaidi ya sisi watanzania kuchukua hatua, kama kufa na tufe woote, haiwezekani mtu mmoja au kikundi cha watu wasio zidi 10 nchi hii, wawe sababu za huzuni, majonzi, machungu, maumivu, chuki, ufukara wa watanzania, alafu tuendelee kupuuza...kama kufa mtuue wote.
Kwa bahati mbaya sana, siku ya kufa kwangu siijui, na pengine imekaribia, kwahiyo vitisho vya kufa ni ubatili mkubwa katika maisha yangu, suala hapa ni ukombozi wa nchi, kama kufa tutakufa tu, na pengine ninyi mnao tuuwa leo au mnao panga haya mauwaji, au mnao fadhili haya mauwaji na ninyi mnao tetea haya mauwaji ya watanzania tu kwasababu ni wapinzani, mnaweza hata msifike hapo ambapo mnaweza kuyashuhudia makubwa ya nchi hii.
hatuwezi kama Taifa kurudi nyuma eti kwasababu, kuna kamanda wa polisi atatupiga risasi za moto kama walivyomfanyia yule mwanafunzi, No way!! Tumechoka. Muda wa kutishanatishana ulisha pitwa na wakati. Mmesahau kwamba, haya mateso ndio msingi wa ujasiri tunao upata wa kukabiliana na ninyi wauwaji?? Tutapambana juu ya haki zetu kama raia na kama watanzania kwa gharama yoyote.
#TanzaniaRevolution #26/04/2018