Petition Closed

@TSNP elimu bora

This petition had 1,984 supporters


Kwa muda mrefu sasa Taifa la Tanzania limekuwa na mfumo wa ELIMU usio rafiki kwa maendeleo ya wanafunzi na Taifa kwa ujumla. Mfumo huu wa ELIMU haumuwezeshi kabisa mwanafunzi kuwa mbunifu na  mwenye uwezo wa kujitegemea katika kukabiliana na mazingira yanayomzunguka. Badala ya kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kutafakari changamoto zinazokabili jamii zetu na kutoa ufumbuzi, mfumo huu huzalisha wataalamu wasio na sifa. Tumetengeneza jamii ya wanafunzi wanaohangaika na kufaulu mitihani tu, ila si kujifunza.

 Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), una sababu kubwa mbili za kuupinga mfumo huu wa sasa:

1)- mfumo huu tumeurithi kutoka kwa wakoloni. Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake alikiri wazi kwamba hakuna mkoloni aliyekuwa na nia ya dhati ya kumkomboa mwafrika. Sisi Mara baada ya kupata Uhuru, tuliurithi mfumo uleule wa ELIMU ya mkoloni, uliokuwa ukimwandaa mwafrika kuwa mfanyakazi wa mzungu. Si ajabu leo wengi wanasoma wakijiandaa kuajiriwa na sio kujiajiri huku wakijua wazi ajira hakuna.

2)- ELIMU inaendeshwa kwa utashi wa waziri aliyeko madarakani. Tumeshuhudia vipindi tofauti vya mawaziri wa ELIMU vilivyojaa mabadiliko lukuki kadri ya wanavyoona inafaa. ELIMU imefanywa jambo la kisiasa na sio la kitaalamu, siku zinavyozidi kwenda matamko yasiyo na msingi kutoka kwa viongozi wetu wa kitaifa yanazidi kuididimiza.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania unapenda jamii ifahamu ya kuwa muathirika mkuu wa mambo yote haya ni mwanafunzi, hivyo kama njia sahihi ya  kuleta mageuzi katika mfumo wa elimu, kutatua changamoto zinazomkabili mwanafunzi na kuelekea Tanzania yenye viwanda,  Mtandao huu unawaomba watanzania kuungana nasi kumtaka mhe.Rais John Magufuli, kuunda tume ya kitaalamu itakayopitia mfumo huu wa ELIMU na kuleta mapendekezo ya mfumo bora zaidi wa ELIMU.

   Tuko tayari kushirikiana na wananchi wote wa Tanzania katika kutimiza adhma hii ya kuleta mageuzi ya mfumo wa ELIMU yetu

,,,,,,, Twende Pamoja na TSNP 2016Today: Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) is counting on you

Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) needs your help with “Mhe. John Joseph Pombe Magufuli: @TSNP elimu bora”. Join Mtandao Wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) and 1,983 supporters today.