KAMPENI HURU YA WANANCHI WA TANZANIA KUDAI KATIBA MPYA, HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA.

KAMPENI HURU YA WANANCHI WA TANZANIA KUDAI KATIBA MPYA, HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA.

0 have signed. Let’s get to 1,500!
At 1,500 signatures, this petition is more likely to get picked up by local news!
WAKA Wananchi&Katiba started this petition to The president of Tanzania and

Sisi Wananchi wa kawaida wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kwa umoja wetu tunaitwa WAKA yaani Wananchi na Katiba; tumeanzisha kampeni hii kwa njia ya mtandao kwa lengo la kushinikiza serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan iweze kurejea mchakato wa katiba mpya kwa misingi ya maoni ya wananchi yaliyo kusanywa na tume ya jaji mstaafu Warioba.

Ili kufikia lengo hilo, tunakusudia kutoa elimu ya katiba mpya kwa wananchi wenzetu, elimu ya uraia, pamoja na haki za binaadam,  kupitia mitandao ya kijamii, na kupitia kampeni maalum tutakayoizindua ya kukusanya saini za watanzania katika mitaa wanayoishi ili kwa umoja wetu tuoneshe dhamira ya dhati ya taifa letu kutaka katiba mpya.

Hivyo kampeni yetu ni ya watanzania wote na haiko chini ya chama chochote cha siasa wala dini yoyote. Kinachotuunganisha ni utanzania wetu na uzalendo wetu. Hivyo sisi ni wananchi tusioegemea mrengo wowote wa kisiasa na wala tusiofungamana na chama chochote cha siasa.Twendeni pamoja, umoja wetu ndio ushindi wetu, usiruhusu maoni au itikadi na msimamo wa chama cha siasa upore uhuru wako wa mawazo na uwezo wako wa kutafakari na kuamua hatima ya taifa lako.

Tunaweka Dai letu kwa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ili aitishe upya bunge la katiba lisilo na wabunge wa Bunge la Kawaida la Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania kwa lengo la kurudia Mchakato wa Katiba Mpya kwa Misingi ya Mapendekezo au Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba.

Tunavishinikiza pia vyama vikuu vya Upinzani Tanzania ACT Wazalendo na CHADEMA waunge mkono madai haya ya katiba mpya.

0 have signed. Let’s get to 1,500!
At 1,500 signatures, this petition is more likely to get picked up by local news!