Petition Closed

We Tanzanians in the Diaspora , Believe That Dual Citizenship is a Great Thing for The Country. Please Support.

This petition had 1,781 supporters


Dual Citizenship ni :

1. Kwa Ajili ya Wewe

2. Kwa Ajili ya Nchi

3. Kwa Ajili Ya Watoto Wako

4. Kwa Ajili Ya Maendeleo ya Nchi

 

The government has said that it is high time now for Tanzania to allow dual citizenships so as to enable the Diasporas contribute to the country’s development in terms of income and expertise.

It has been said that many wealthy and well educated Tanzanians living abroad fail to contribute to national development because they are denied the right to dual citizenship.

The Minister for Foreign Affairs and International Co-operation Bernard Membe said this when he was launching a new outreach project for Tanzanians living abroad prepared by the Tanzanian Diaspora department and International Organisation for Migration (IOM) called on all citizens, politicians and academics to support the inclusion of dual citizenship in the new constitution. 

Uraia wa nchi mbili au uraia pacha ni jambo ambalo limekuwa likijadiliwa na Watanzania wanaoishi kwenye diaspora kwa muda mrefu sasa. Kwa vile kipindi hiki ndicho kipindi cha kujadili masuala ya katiba mpya, Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wameonelea umuhimu wa kuandika waraka huu ili kulitetea suala la uraia pacha na kuhakikisha linaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kabla ya kuanza kulijadili suala la uraia pacha kama Watanzania tunaoishi nje ya Nchi yetu tungependa kutambua masuala yafuatayo:

Kwanza kabisa, kama Watanzania wanaoishi kwenye diaspora, tunatambua jitihada za dhati za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali ya Awamu ya Nne kutambua mchango wa wana-diaspora katika maendeleo ya nchi. Hii imedhiirishwa kwa kuanzishwa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kuteuliwa Mkurugenzi kukiongoza ili kurahisisha mahusiano na utengenezaji wa Sera na mikakati inayowahusu wana-Diaspora.

Pili, tunatambua mchango wa Serikali katika kuhamasisha uundwaji wa Jumuiya za Watanzania nje ya nchi kama njia bora ya kuwaunganisha Watanzania kujadili mambo muhimu kwa nchi yao na maslahi yao. 

Tatu, tunatambua mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuwasilisha maoni ya wana-diaspora kwa Tume ya Katiba ili yafikiriwe na kuwekwa ndani ya Katiba Mpya. Na ni matumaini yetu kuwa wizara hii na taasisi nyingine husika zitashirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa suala la uraia pacha linawekwa kwenye Katiba mpya ya Tanzania.

Nne, mchango wetu kama Watanzania wanaoishi kwenye diaspora ni mkubwa sana katika kuendeleza uchumi wa Tanzania. Kwa mfano, mwaka wa 2012 Watanzania waishio nje ya nchi walituma pesa kiasi cha dola milioni 250 kwenda Tanzania. Idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi wanakisiwa kuwa asilimia 5 ya Watanzania wote, yaani karibia watu milioni 2.25 (Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje). Na kiasi cha fedha zinazotumwa Tanzania kutoka kwenye diaspora kinazidi kuongezeka siku hadi siku. 

Tukirudi kwenye mada kuu ya waraka huu ambayo ni ya uraia pacha, swali la kujiuliza ni nini hasa umaana wa uraia pacha? Mtu aliye na uraia pacha ni mtu ambaye anatambulika na serikali zaidi ya moja kuwa raia wa nchi husika. Wakati mwingine mtu mmoja anaweza kuwa raia wa nchi zaidi ya moja bila hata ya yeye kufahamu, lakini katika ufahamu wetu kama Watanzania waishio kwenye Diaspora, uraia pacha unatokana na mtu husika kuchagua kuwa na uraia pacha au mhusika huyu anakuwa raia kulingana na sheria za nchi husika kutokana na sababu muhimu zifuatazo:

 

  1. Kwanza, Mhusika ameomba uraia katika nchi ya nje na akakubaliwa kuwa raia wa nchi hiyo; 
  1. Pili, nchi aliyozaliwa Mhusika ni nchi ambayo inatoa uraia kwa mtu yeyote aliyezaliwa nchini humo;

 

  1. Tatu, mhusika ana wazazi waliozaliwa katika nchi nyingine tofauti na ile  aliyopata uraia kwanza na nchi ile inaruhusu watoto wenye wazazi au babu na bibi raia wa nchi hiyo kuwa raia; 
  1. Nne mtu aliyeoa au kuolewa na raia wa nje anaweza kupewa uraia kutokana na  sheria za nchi husika; 
  1. Tano, mhusika anaweza kupata uraia pacha baada ya kukaa kihalali katika nchi nyingine kwa muda mrefu unaokubalika kisheria.

Hayo yote ni masuala ambayo yanaweza kumpa uraia pacha Mtanzania anayekaa kwenye nchi nyingine. Suala la uraia pacha vile vile lina historia yake. Kwa mfano, mwezi Septemba 2013 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipata fursa ya kuzungumza na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa New York na Vitongoji vyake.

Mheshimiwa Rais Kikwete alisisitiza kuwa kuna haja ya wanadiaspora kuwaelimisha Watanzania wenzao kuhusiana na suala hili, lakini vile vile kuna haja ya wanadiaspora kuwa na sauti moja na kulileta suala hili serikalini.Today: Mickey "MIKIDADI" John is counting on you

Mickey "MIKIDADI" John Amos needs your help with “Honourable Bernard Membe: We Tanzanians in the Diaspora , Believe That Dual Citizenship is a Great Thing for The Country. Please Support.”. Join Mickey "MIKIDADI" John and 1,780 supporters today.