Petition Closed

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani Ajiuzulu

This petition had 1,543 supporters


Sisi, watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaamini na tumetambua kuwa kuna uzembe na kutowajibika kwa Waziri wa Maambo ya Ndani Tanzania, Mh Dokta Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Jeshi Polisi Nchini, Inspekta Jenerali Simon Sirro katika kushughulikia masuala yanayoweza kuhatarisha usalama wa Watanzania.


Katika siku za hivi karibuni, vitendo vya mauaji ya raia wasio na hatia vimeongezeka, mbele ya macho ya wengi hakuna juhudi za dhati ambazo zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kukomesha vitendo hivyo.

Septemba 7, 2017 mchana, Gari la Mbunge wa Upinzani Mh Tundu Lissu lilirushiwa risasi 38 huku zaidi ya risasi 18 zikipata sehemu mbalimbali za mwili wake. Ikiwa ni zaidi ya miezi mitano baada ya tukio lile, hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola.

Katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 26, 2017, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu (LHRC) lilibaini kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binadamu ulioripotiwa kufanywa na vyombo vya dola, watu wasiojulikana na wafuasi wa vyama vya siasa, vitendo hivi vinajumuisha watu kupigwa, kukamatwa na kujeruhiwa lakini hadi sasa, Februari mwaka 2017 wahusika hawajachukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola ikiwamo mahakamani.

Tarehe 12, Februari 2018, kiongozi wa CHADEMA kata ya Hananasif, Daniel John aliuawa kinyama kwa kushambuliwa na mapanga na kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa bahari.

Tarehe 16, Februari 2018, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji, Aquilina Akwilini aliuawa kwa risasi wakati ambao jeshi la polisi lilirusha risasi kuwatawanya waandamanaji wa amani wa CHADEMA waliokuwa wakielekea ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni kudai barua ya utambulisho wa mawakala wao katika uchaguzi wa marudio wa Ubunge, jimbo la Kinondoni.

Pamoja na hayo, vitendo vya utekaji na kupotea kwa wanasiasa na waandishi wa habari vimeendelea, kuokotwa miili ya watu waiofahamika ikiwa imetupwa baharini limekuwa ni jambo endelevu, na mauaji dhidi ya askari wa jeshi la polisi yameongezeka ndani ya miaka miwili kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu, ingawa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh Dk. Mwigulu Nchemba amendelea kukalia kiti chake bila kuwajibika au kuwajibishwa na mamlaka husika.

Hivyo basi, sisi watu wa Tanzania tunamuomba Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Pombe Magufuli kumuondoa kazini Waziri wa Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kama Waziri anayesimamia chombo cha Ulinzi wa Raia na Mali zao, Jeshi la Polisi Tanzania. Pia, tunamuomba Mh Rais Dk John Magufuli kuchukua hatua, ikiwemo kumfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Simon Sirro ikiwemo na kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, ni kurudisha uwajibikaji katika mfumo mzima wa kusimamia ulinzi na usalama wa watanzania.

 

We demand Mwigulu Nchemba’s Resignation as Minister for Home Affairs.

We, as citizens of the United Republic of Tanzania, due to recent events believe and have witnessed immense lack of accountability and taking of action by home affairs minister, Mwigulu Nchemba and are hereby calling on him and the Inspector General of Police Simon Sirro to IMMEDIATELY resign.

There has been an increase in the number of murder cases on innocent civilians, the disappearance of political party members and media personnel, shooting of a prominent politician in broad daylight. As a nation, we are yet to see efforts in apprehending the perpetrators of such violent crimes that are indeed the new the norm in Tanzania.

Legal Human Rights Center (LHRC) reported on violation of human rights by authorities during the LGA by-elections held on 26th November 2017. We are yet to see justice served on the violators, none have been apprehended neither taken to court. Tundu Lissu’s assassination attempt is yet to see an update on who pulled the many triggers. The ongoing investigation has yielded no reassuring results.

On 12th February 2018, Daniel John, a CHADEMA Cadre, Hananasif Ward, was brutally murdered by machetes, skull fractured by a heavy object. His body was found along the sea side.

16th February 2018, Aquilina Akwilini was shot dead by a stray bullet, one that was fired by the police to disperse a crowd that was peacefully marching to the Director of Elections, albeit unlawfully. The march as claimed by CHADEMA was to claim their right to have their poll agents present in the Kinondoni Constituency re-elections. None of them marchers were armed. Aquilina was not in the march, she was getting off a bus probably to go back to school. She had just started her first semester University exams.

Missing persons reports have been filed, families are yet to receive any news on the whereabouts of their loved ones. Dead bodies have floated ashore with no reports on identifying them or where they came from. We have also heard of increased police officer killings in the past two years more than ever in Tanzanian history.

Mwigulu Nchemba continues to sit on his ministerial seat as if nothing is happening, and his statements have left us with more questions than answers. We do not have faith in you, we do not have faith in your leadership, we do not have faith in your tactics. We are tired of being killed and loosing loved ones.

Therefore, We, as signed by every Tanzanian in this petition, appeal to President Dr John Joseph Pombe Magufuli to demand your immediate resignation and that of the Inspector General of Police Simon Sirro, and that of Dar es Salaam Police Comissioner Commander Lazaro MambosasaToday: Joseph is counting on you

Joseph Rwegasira needs your help with “HE President John Pombe Magufuli: Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani Ajiuzulu”. Join Joseph and 1,542 supporters today.