Petition Closed

Vifo Barabarani

This petition had 38 supporters


Chini ya mwezi mmoja visa vya ajali barabarani vimeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini huku vifo vya wananchi zaidi ya hamsini na watano vikiripotiwa maeneo tofauti. Hali hii imesikitisha mno ikikumbukwa kuwa waliopoteza maisha ni wanajamii wanaotegemewa kwa namna moja au nyingine. Miongoni mwao pia ni watoto waliokuwa na ndoto za kutimiza maishani mwao.

Tarehe tisa ajali ilitendeka kwenye barabara kuu ya Nakuru Eldoret iliyosababisha vifo vya wazalendo wasiopungua saba wakiwemo wanamziki wa bendi maarufu ya Kenene. Siku kadhaa baadaye ajali nyingine ikatokea kwenye daraja kuu la barabara ya Kamuywa Bungoma ambayo ilisababisha vifo vya watu kumi na tisa baadhi yao wakifia hospitali wakipokea matibabu. Kilichohuzunisha zaidi ni kuwa familia moja katika gatuzi la Vihiga ilipoteza watu tisa katika ajali hiyo.

Ajali ya hivi punde imetendeka eneo la Salgaa na wananchi wengi wamepoteza maisha yao miongoni mwao wakiwemo wanandoa wawili waiokuwa wakirejea nyumbani baada ya kuhudhuria sherehe za kukuzwa kwa mahafali chuo kikuu cha Jomo Kenyatta. Matukio haya yanahuzunisha mno kwa kuwa yameathiri jamii husika moja kwa moja.

Bwana Rais nitakuomba kwa heshima na taadhima utusaidie katika kulipiga jeki swala hili la usafiri barabarani. Neno lako litatosha kuleta mabadiliko kwenye sekta hii. Hata hivyo ninayo mapendekezo ambayo yakizinatiwa yataimarisha usalama barabarani:

1. Upanuzi wa barabara ufanyike katika baadhi ya maeneo nchini. Kunazo barabara ambazo ni ndogo mno kiwango cha kuleta taharuki magari yanapopitana barabarani.

2. Sheria kali kubuniwa dhidi ya madereva wanaopuuza sheria za barabarani. Hii itawezesha kuimarisha nidhamu barabarani miongoni mwa madereva wanaoendesha magari kwa kasi mno na wanaoendesha wakiwa wamelewa.

3. Polisi wa Trafiki waimarishe kazi zao barabarani. Baadhi yao wachunguzwe ili wasiruhusiwe kula rushwa na kukubali magari kupita bila kutathminiwa kwa kina.

4. Baadhi ya barabara zitengewe magari makubwa(matrela) na nyingine zitumiwe na magari ya kawaida. Hii itasaidia kupunguza msongamano wa magari na ajali. Ikumbikwe baadhi ya ajali zimesababishwana magari haya yanayotumia barabara moja.

5. Katika maeneo ya magharibi, magari ya kupakia na kusafirisha miwa yasiruhusiwe kufanya shughuli zao usiku. Baadhi ya magari haya yamesababisha ajali nyingi mno nyakati za usiku.

Hili ni tatizo la jamii linalotuathiri sisi sote. Yafaa tulikabili vilivyo kabla halijatuzidi. Macho ya wananchi yanakutazama Rais yakiwa na matumaini kutoka kwako. Kama nilivyosema hapo awali, neno lako litatupa matumaini.

Shukrani za dhati.Today: Gabriel is counting on you

Gabriel Ing'ahu needs your help with “Change.org: Vifo Barabarani”. Join Gabriel and 37 supporters today.